Uongozi wa klabu ya Dodoma Jiji FC itakayoshirik Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, umeanika hadharani orodha ya wachezaji waliosajiliwa na klabu hiyo, tayari kwa Mshike Mshike wa kusaka alama tatu muhimu kuanzia Septemba 06.
Dodoma FC ambayo ndio bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2019/20, imefanya usajili wa wachezaji kadhaa, na kuwaacha wachache waliokuwa nao kwenye harakati za kupanda Ligi Kuu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa klabu hiyo, Ramadhani Juma ‘Raju’, ametangaza wachezaji watakaounda kikosi chao, ambapo upande wa walinda mlango ni makipa Hussein Masalanga, Emmanuel Mseja na Aron Kalambo aliyesajiliwa kutoka Prisons akitoka kucheza kwa mkopo KMC.
Mabeki waliwatajwa ni Anderson Solomon, Aboubakar Ngalema, Ibrahim Ngecha, Mbwana Kibacha, Hassan Kapona, George Wawa aliyesajiliwa kutoka Singida United, Jukumu Kibanda aliyesajiliwa akitokea Namungo FC, Augustino Ngata na Justine Omari.
Viungo: Rajab Seif, Jamal Mtegeta, Omari Kanyoro, Deus Kigawa, Salmin Hoza aliyepelekwa kwa mkopo kutoka Azam FC, Cleophace Mkandala aliyesajiliwa kutoka Prisons, Pter Mapunda aliyesajiliwa kutoka Mbeya City, na Dickson Ambundo kutoka Gor Mahia ya Kenya.
Washambuliaji: Anuary Jabir, Khamis Mcha kutoka Lipuli, Santon Thomas, Seif Karihe ambaye ni straika wa zamani wa Azam na Ruvu Shooting, na Mnaigeria Miachael Chinedu kutoka Alliance FC.