Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa mchujo wa kikosi hicho unafanywa kiufundi na benchi la ufundi lililo chini ya Youssouph Dabo raia wa Senegal.

Kocha huyo bado hajaanza kazi licha kutambulishwa mapema katika kikosi hicho kilichokuwa chini ya Kali Ongala ambaye jana Alhamisi alitangazwa kuachwa na klabu hiyo.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa mchujo wa wachezaji kwenye kikosi hicho unafanywa kitaalamu na benchi la ufundi chini ya Dabo.

“Ni benchi la ufundi litafanya tathimini yake na kwa kile ambacho watapendekeza kitafanyiwa kazi chini ya kocha mkuu Dabo ambaye yupo na anafuatilia timu kila hatua.

“Anapitia video za wachezaji wote wa Azam kwenye mechi ambazo tunacheza na amekuwa pamoja na timu kwenye mechi za ushindani hivyo tunaamini anajua kile ambacho anahitaji kwenye timu yetu kwa msimu ujao.”

Tayari Azam FC imetangaza kuachana na nyota wake kadhaa ikiwa ni pamoja na Rodgers Kola, Keneth Muguna, Ismail Aziz na Bruce Kangwa.

Mbwana Makata: Nina deni kubwa Ruvu Shooting
Polisi wakamata mamia ya mifugo, watuhumiwa 153 mbaroni