Leo Bungeni jijini Dodoma Spika wa Bunge Job Ndugai amemtoa nje mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali mara baada ya mbunge huyo kushundwa kuzuia hisia zake pindi alipokuwa akitaka kutoa hoja juu ya suala la ushuru wa korosho.
Ambapo kulitokea mvutano mkali baina yake na Spika Ndugai na kuamua kuchukua uamuzi wa kumtoa nje ya Bunge pindi kikao cha Bunge kikiwa kinaendelea.
Bobali amesema alisimama kupingana na maelezo aliyokuwa anayatoa Mbunge wa Siha Dk Godwin Mollel (CCM) ambaye anaunga mkono hoja inayodai kuwa ushuru wa korosho kupelekwa serikali na kudai kuwa analipotosha bunge.
Alipohojiwa na Chombo cha habari Bobali amesema
”Nilishindwa kuvumilia ndio maana nilitaka kumpa taarifa Dk Mollel kuhusu ukweli wa masuala ya korosho Sikupendezwa na maelezo yake wakati wa mjadala wa muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2018.
Aidha amesma anamshukuru Mungu kwa kumuepusha kuwa sehemu ya watu waliopitisha sheria hiyo ambayo ameona inakwenda kuua korosho hasa kwa watu waliopo kusini.