Idadi ya watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro na kufika katika kilele cha Afrika imeongezeka toka watalii 4  kwenye mwezi wa Aprili na kufikia 420 kwa mwezi Agosti .

Afisa hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro , Charles N’gedo amesema kuwa toka kuondolewa kwa katazo la mlipuko wa Covid-19 watalii 657 wamefanikiwa kupanda Mlima Kilimanjrao .

“Kabla ya mlipuko wa virusi vya corona walipokelewa watalii 1544 katika mwezi wa Machi lakini baada ya  nchi nyigi kufunga mipaka yao ,idadi ikapungua . Mwezi wa nne tulipokea watalii 4 , mwezi mei wageni 3,” alisema N’gendo

Aliongeza kuwa mwezi juni walikuja 24, na mwezi julai idadi iliongezeka na kufikia watalii 206 waliopanda mlima Kilimanjaro .

Kati ya watalii wote aliopanda mlima kwenye miezi mine iliyopita ,207 walitoka jumuhia ya Afrika Mashariki ,52 walikuwa wageni ambao ni wakazi wa Tanzania,na 442 walikuwa ni wanafunzi .

Idadi hii imeongezeka sambamba na mashirika ya ndege ya KLM,Qatar na Ethiopia kutangaza kuogeza safari zake kwenye ardhi ya Tanzania . 

Shinyanga, Geita vinara wa RAMLI
Keita aruhusiwa hospitali

Comments

comments