Klabu ya Manchester United inamkomsa kiungo wake Paul Pogba ambaye alipata maumivu ya misuri ya na kuna taarifa kuwa mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja hadi msimu wa sikukuu za Christmass.

Pogba anaweza kukosa michezo ambayo Man Utd itakabiliana na Chelsea, Tottenham na pia anaweza kukosa mchezo wa Manchester Derby dhidi ya City.

Wakati mashabiki wa United walishaanza kumsahau Paul Pogba kutokana na kiwango kizuri sana cha Mourruane Fellaini kumekuja taarifa kwamba Fellaini ni majeruhi na anaweza kukaa nje kwa miezi kadhaa.

Fellaini ameumia wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ubelgiji huku kocha wake Roberto Martinez akisisitiza kwamba wana mashaka makubwa kuhusu majeraha ya Fellaini, hii leo taarifa kamili ya majeraha ya Fellaini inaweza toka lakini inatarajiwa kuwa mbaya sana kwa United.

Manchester United wamekuwa na msimu mzuri sana tangu msimu wa 2017/2018 kuanza lakini sasa jinamizi lililowaandama msimu uliopita la majeruhi linaonekana limerudi tena Old Traford kwa mara nyingine.

Video: Meya Kinondoni awafuta machozi wananchi wake
Mji mkuu wa Ghana wakumbwa na mlipuko mkubwa wa gesi