Muigizaji kiongozi wa kike kwenye series ya Empire iliyotingisha ulimwengu wa filamu duniani katika kipindi cha hivi karibuni, Taraj P. Henson maarufu kama Cookie Lyon ameelezea furaha yake baada ya kutajwa kuwania tuzo za Emmy mwaka huu.

Muigizaji huyo maarufu aliyejiongezea mara dufu umaarufu huo kwa ushiriki wake kwenye series hiyo alielezea hatua hiyo kuwa ni jambo lililomfurahisha sana na kuamini kuwa amewagusa watu wengi zaidi kupitia kipaji chake

The fact that I am getting nominated, that is amazing … I am honoured, I am pleased. But what that represents for me is I’ve touched even more people through my talent, with the gift that God gave me,” Alisema Henson said.

Ingawa muigizaji huyo anapata ushindani mkali kupitia kipengele hicho, mashabiki wanampa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika tuzo hizo.

Taraj anashindania tuzo ya Emmy katika kipengele cha ‘Outstanding Lead Actress in a drama series’ pamoja na waigizaji wengine wakubwa wa kike kama Viola Davis (How to Get Away With Murder) , Claire Danes  (Home Land), Elisabeth Moss (Mad Men), Robin Wright (House of Cards) na Tatiana Maslany (Orphan Black).

Mashabiki wa ‘Empire’ wanausubiri kwa hamu msimu wa pili wa series hiyo unaotarajiwa kuanza rasmi September 24, 2015. Tayari vionjo vya msimu huo vimeanza kuoneshwa.

Joh Makini Aeleza Sababu Za Kutojihusisha Na Kampeni Za Siasa
Mnaomfuata Rihanna Mnapotea, Mwenyewe Anaonesha Njia Hapa