Mwenyekiti wa Kamati  ya Nidhamu ya Simba, Kamanda mstaafu Suleiman Kova ameeleza ni kwanini kamati yake imependekeza mchezaji Jonas Mkude kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Mhimbili kwa ajili ya vipimo vya Afya.

“Tumeona kutoa hukumu pasipo kujua tatizo lake kitabibu haitakuwa sawa, anapaswa kuhukumiwa kulingana na tatizo lake kiafya kama watakavyotuelekeza madaktari.”

“Hospitalini huwa wanaangalia mambo mengi  yanayosababisha tabia kama hizi; Saikolojia, msongo wa mawazo, utumiaji sugu wa vinywaji vikali na mambo mengine, maana huyu ni binadamu , majibu yatakayotoka ndiyo yataelekeza hukumu yake iwe ya namna gani.

“Mkude ni Kijana bado anahitaji kusaidiwa ndio maana adhabu yake itategemea na taarifa ya daktari.

Manyama asaini miwili Simba SC
Gomes kushusha kifaa Simba SC