Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli leo alimtembelea na kumjulia hali waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye aliyelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Taasisi ya Jakaya Kikwete.

Sumaye amelazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku nne akisumbuliwa na tatizo la moyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Madaktari wanaomtibu wamemueleza rais Magufuli kuwa afya yake inaendelea kuimarika.

Sumaye na Magufuli2

Akiongea baada ya kuzungumza na rais, Sumaye alieleza kuwa alikuwa hajataarifiwa kama rais Magufuli angeenda kumtembelea hospitalini hapo.

Sumaye na Magufuli3

“Hili ni jambo kubwa sikutegemea, ndio maana nilikuwa kama nimeshtuka. sikutegemea na sikupata taarifa yoyote kabla. Kama ulivyoona niliona watu wanaingia, kushtuka namuona mheshimiwa rais. Namshukuru sana rais Magufuli kwa kuwajali watu wake. Hivi sasa afya yangu ni nzuri, naendelea vizuri, natumaini katika siku chache zijazo nitatoka hapa hospitali,” alisema Sumaye.

Rais Magufuli alimuombea Sumaye apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

2 Face Idibia abadili jina, Angalia hapa jina lake jipya
FIFA Yaitaka Etoile Du Sahel Kuilipa Simba Haraka