Mwanamuziki mahiri mshindi wa tuzo kadhaa barani Afrika Zahara kutoka Afrika kusini amefariki dunia.

Nyota huyo amefia katika hospitali ya binafsi alipokuwa akipatiwa matibabu huko mjini Johannesburg Jumatatu usiku.

Hitmaker huyo wa Loliwe alilazwa hospitalini kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya Ini yaliyobainishwa na familia takriban wiki mbili zilizopita na kwa mujibu wa chanzo cha karibu inaelezwa kuwa mwimbaji huyo alifariki dunia kabla ya saa tisa alasiri.

Zizi Kodwa, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, alichapisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X/Twiter ujumbe uliosomeka: “Nimehuzunishwa sana na kifo cha Zahara. Pole zangu za dhati kwa familia ya yake na tasnia ya muziki ya Afrika Kusini”

“Serikali imekuwa na familia kwa muda sasa. Zahara na gitaa lake alifanya mambo ya makubwa na ya kudumu katika muziki wa Afrika Kusini,” alisema Kodwa.

Wiki moja iliyopita, familia ilithibitisha kuwa Zahara alilazwa hospitalini kwa wiki moja.

Waliwashukuru wale waliowaunga mkono na kushirikiana na mwanamuziki huyo katika kipindi chote alichokuwa akipatiwa matibabu, Hii ni mara baada ya ripoti kwamba mwimbaji huyo alikimbizwa hospitalini kutokana na “matatizo ya Ini”.

Zahara alilazwa katika wodi ya kawaida lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi ICU alipokuwa akipatiwa matibabu wa kuangalizi maalumu mpaka umauti ulipomfika.

Hit, albamu na tuzo
Katika kipindi cha uhai wake, Zahara alitoa albamu tano za muziki zilizofanikiwa kuuza kwa kiwango kikubwa, kuanzia Loliwe (2011) hadi Nqaba Yam (2021), zote zilishika nafasi ya kwanza kwenye iTunes.

Amejinyakulia Tuzo 17 za Muziki huko Afrika Kusini , pamoja na Tuzo tatu za Metro FM na Tuzo moja ya Burudani kutoka nchini Nigeria.

BOFYA HAPA KUTAZAMA MOJA YA WIMBO MAARUFU WA ZAHARA

Mila: Wanakata Vidole kuifurahisha mizimu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 12, 2023