Rai wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Novemba 19 ameteua Baraza jipya la Mawaziri Zanzibar.

Teuzi alizozifanya Rais Mwinyi mpaka sasa ni:-

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji – Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora – Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Dokta Khalid Mohammed Salum. 

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo –  Soud Nahodha Hassan. 

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni – Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi – Riziki Pembe Juma.

10. Wizara ya Maji na Nishati – Suleiman Masoud Makame.

11. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Lela Mohammed Mussa.

12. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Mheshimiwa Abdallah Hussein Kombo. 

13. Wizara ya Ujenzi – Mheshimiwa Rahma Kassim Ali.

14.Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri. 

15. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

Katika baraza hilo la Mawaziri hadi sasa hakuna Wizara ambayo ina Naibu Waziri, na nafasi mbili za Mawaziri ambazo ni kutoka wizara ya Afya na Wizara ya Biashara zimeachwa wazi kwa ajili ya Chama cha ACT- Wazalendo.

Mwinyi awaachia ACT-Wazalendo Wizara mbili
Hitimana Thiery aondoka Namungo FC