Baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kuwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 leo wabunge wameanza kujadili bajeti hiyo.

Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa leo Juni 14, 2021 amekuwa mchangiaji wa kwanza, Bungeni Dodoma wakati wa kujadili Bajeti ya Serikali Kuu iliyosomwa Juni 10, 2021.

Ambapo ameeleza kuwa bajeti iliyowasilishwa imekuja kujibu swali ambalo watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusiana na miradi ya kimkakati ambapo imeelezwa kuwa hakuna mradi utakaokwama wala kusimama hata kwa mwezi mmoja.

“Kila siku hapa bungeni hakukosi swali la Wizara ya Maji na hisia za wabunge zilijionesha sana wakati wa bajeti ya Wizara ya Maji. Bajeti hii imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji. Kwenye majimbo yetu pamoja na ujenzi mkubwa wa miundombinu ya afya, vituo vya afya, vifaa tiba wataalamu na madawa. Bajeti hii imekuja na mwarobaini wa kutatua kero za afya” amesema Silaa

Bilioni 1.5 zatengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa
Mahakama yaahirisha hukumu ya Mdude wa Chadema