Shirika la kusambaza umeme nchini Kenya – KPLC limetangaza kupotea kwa nguvu za umeme katika sehemu nyingi za Taifa hilo.
Taarifa ya KPLC inaeleza kuwa kupotea kwa umeme kumesababishwa na hitilafu za Mitambo huku Wahandisi wao wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Aidha, nguvu za umeme pia zimepotea katika Kwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyattta – JKIA, jijini Nairobi.