Kocha Hitimana Thiery amemtaja kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar Vicent Barnabas, kuwa sababu za kusitisha mpango wa kuendelea kufanya kazi kwenye klabu hiyo, ambayo ipo kwenye mazingira mabaya ya kushuka daraja.

Hitimana aliweka wazi mpango wa kuachana na Mtibwa Sugar usiku wa kuamkia jana Jumatano (April 07), akiwa nchini kwao Rwanda alipokwenda kwa ajili ya mapumziko.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuzinoa klabu za Biashara United Mara na Namungo FC amesema tangu alipoanza kazi Mtibwa Sugar, amekua hana maelewano mazuri na Vicent Barnabas.  

Hitimana amesema: “Nimeamua kuondoka Mtibwa Sugar kwa sababu tukishindwa kuelewana na Kocha Msaidizi wa timu hiyo Vicent Barnabas.”

“Tulianza kutokuelewana Kutoka tukiwa Mapinduzi Cup Zanzibar na tokea hapo Kocha Msaidizi Vicent Barnabas alitaka kufanya mabadiliko kwenye timu yetu siku tunacheza dhidi ya Simba SC.”

“Nilitaka kuondoka Mtibwa Kutoka Mwezi wa kumi na Mbili Maana niliona mambo hayaendi ila nikavumilia pamoja na kunilipa stahiki Vizuri ingawa nilikuwa sijasaini Mkataba nao.”

“Nimeona nikae pembeni Ili kuinusuru timu Maana niliona kuna msuguano Kati yangu na Msaidizi wangu, Pamoja na kuripoti kwa uongozi ila sikuona hatua madhubuti zilizochukulia na Uongozi wa timu.”

“Msaidizi wangu Vicent Barnabas alikuwa ana wagawa Wachezaji wa timu ya Mtibwa Maana alitaka kuwa Kocha Mkuu. Nikaona ili kuinusuru hii timu kubaki ligi Kuu inabidi Mimi niondoke na ukweli sasa nimeondoka na siwezi kurudi Mtibwa kwa Sasa.”

Ikumbukwe kuwa Vicent Barnabas alikabidhiwa kikosi cha Mtibwa Sugar kwa muda, baada ya kuondoka kwa kocha Zubery Katwila ambaye alitimkia Ihefu FC mwishoni mwa mwaka 2020.

Baada ya kuajiriwa kwa Hitimana Thiery, Vicent Barnabas aliendelea na majukumu yake kama kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar.

SADC yaitisha Mkutano wa dharura, Rais Mwinyi amwakilisha Rais Samia
Billioni 1.5 kuwanufaisha wasanii