Kituo cha redio cha Hitz Fm kilichoko visiwani Zanzibar kimechomwa moto na watu ambao bado hawajajulikana.

Mtangazaji wa zamu aliyekuwa akiongoza matangazo wakati huo, Ally Abdullah amesema kuwa kundi la watu takribani 20 walivamia kituo hicho na kumkuta akiendelea kurusha matangazo kisha kumuwekea panga shingoni.

Abdullah alieleza kuwa watu hao walimumteka kwa kumuwekea panga shingoni wakitishia kumkata endapo hatazima redio hiyo kwa hiari na kufuata maelekezo yao.

Abdullah aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimika kufuata maelekezo ya watu hao waliomfunga kamba kabla ya kukichoma kituo hicho hadi kuteketea kwa moto kabla ya kutokomea.

Naibu Kamishna wa Polisi Zanzibar, Salum Msangi alieleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 7 na dakika 40, usiku wa kuamkia leo.

Bado haijafahamika sababu ya watu hao wasiojulikana kukichoma moto kituo hicho.

Magaidi Wa IS Watishia Kumuua Papa, Papa Azungumzia Tishio Hilo
Mwanasheria Mkuu Awakana Wakuu Wa Mikoa Wanaositisha Likizo Za Watumishi