Hatimaye Benchi la Ufundi la Simba SC limefunguka sababu za kumuachwa jijini Dar es salaa kiungo kutoka Zambia Clatous Chotta Chama.

Chama hakuonekana kwenye msafara wa kikosi cha Simba SC uliokua unaelekea Dodoma jana Ijumaa (Januari 20), hali iliyoibua Sintofahamu kwa wadau wa Soka la Bongo, wakihoji kulikoni, kiungo huyo amaeachwa?

Akizunguza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma, Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema, Chama amelazimika kubaki jijini Dar es salaam, kutokana na sababu za kuwa majeruhi.

Mgunda amesema Chama alikua katika hali mbaya kiafya tangu waliporejea kutoka Dubai, lakini alilazimika kucheza dhidi ya Mbeya City baada ya kuthibitika ana uwezo huo.

“Nataka niliweke wazi hili, Chana anaumwa, Chama ni mgonjwa, Chama wakati tunacheza mchezo huo hakuwa anajihisi vizuri, tangu tumetoka safari.”

“Alikua na Fluu na Malaria, kwa hiyo tulimwambia acheze, lakini tuliona kwamba tulikua tunampa mzigo ambao hakustahili, na kwenye haki ya mtu ni kuheshimu haki yake kama binaadamu mwingine.”

“Hata kutolewa kwake katika mchezo wetu na Mbeya City kulisababishwa na hilo, kwa hiyo jamani hatuwezi kumtangazia kila mtu,”

“Halafu tukubaliane Robertinho ni Kocha Mkuu, ana maamuzi ya kufanya lolote, ieleweke kuwa hakuna Kocha yoyote anayemkataa mchezaji mzuri, hakuna, sijawahi kumuona, na ukimuona Kocha wa namna hiyo ujuwe kuna sababu, na sababu ndiyo hiyo niliyoisema.” amesema Mgunda

Simba SC kesho Jumapili (Januari 22) itacheza mchezo wake wa Mzunguuko wa 21 wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji FC itakayokua nyumbani Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, saa moja jioni.

Robertinho: Tunatakiwa kuonesha ukubwa wetu
Dani Alves apoteza kazi Mexico