Serikali ya Uganda, imezifunga shule za nchini humo kabla ya mwisho wa muhula ili kuzuia kuenea kwa kwa ugonjwa wa Ebola, huku ikiendelea kupambana na milipuko katika maeneo yaliyoathiriwa.
Hata hivyo tangazo hilo linakinzana na msimamo wa viongozi wakuu wa nchi kwamba hali ya ugonjwa huo imedhibitiwa ambapo baadhi ya maeneo bado yametajwa kuwa na ugonjwa huo.
Katika miezi miwili iliyopita, watu 55 wamekufa na virusi hivyo na kuna uwezekano wa vifo 22 vya Ebola kabla ya mlipuko huo kutangazwa rasmi mnamo 20 Septemba.
Baadhi ya wataalam, wameelezea kuridhishwa kwao na hatua ya kufungwa kwa shule, wakisema kuwaweka wanafunzi ndani kwa wiki nyingine mbili itakuwa njia bora ya kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo.