Meneja wa Mabingwa wa Soka nchini England Man City Pep Guardiola amedai viwango vya wachezaji wa timu yake vitashuka baada ya mafanikio ya msimu uliopita.
Bosi huyo wa City amekubali timu yake haitaweza kufikia kiwango kilichowafanya kutwaa mataji matatu msimu uliopita (Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya).
“Sidhani kama tutakuwa bora kama msimu uliopita,” alisema Guardiola, ambaye timu yake jana usiku ilianza harakati zake za kusaka taji la sita la Ligi Kuu England kwa kucheza dhidi ya Burnley.
“Ni lazima kidogo. Tutajaribu kuizuia iwezekanavyo. ameshajaribu, katika miezi minne, kujaribu kufanya kile ambacho tumefanya kila msimu.”
Guardiola pia hataki kuweka malengo yoyote kwa Erling Haaland katika msimu wake wa pili kwenye klabu hiyo.
Raia huyo wa Norway, alifurahia mwaka wake wa kwanza, akifunga mabao 52 katika mechi 53 pekee.
Guardiola alisema: “Nitamshauri, asiweke shinikizo kwenye mabao. Nilimwambia Erling, rudà ukiwa bora, kimwili na kiakili. Ukifunga, sawa. Ikiwa hutafunga ni sawa pia.”
Wakati huo huo Man City imeanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu ya England kwa kuichapa Burnley mabao 3-0, usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Agosti 12).