Watafiti wa Chuo Kikuu cha Leicester nchini England wamesema wamegundua kuwa sauti za injini, honi na ving’ora vinavyowafikia watu wanaoishi karibu na barabara zenye magari mengi zinaweza kusababisha shinikizo lao la damu (presha) kuongezeka.

Mhadhiri wa magonjwa ya mazingira katika Kituo cha Leicester cha Afya ya Mazingira na Uendelevu, Samuel Y Cai, amesema uchunguzi huo wa awali haukuweka wazi kwa namna gani kelele au uchafuzi wa hewa unaathiri shinikizo la damu ambapo hata hivyo wanasema utafiti huo mpya unaweza “kubadilisha mambo” ambao unaweza kuathiri sera zijazo za mazingira.

Amesema, “Uchunguzi huu ni wa kwanza nchini Uingereza ambao ulichunguza moja kwa moja athari za kuwepo kwa kelele za muda mrefu kwenye foleni na misongamano ya barabarani na tishio la matukio ya shinikizo la damu katika kipindi cha ufuatiliaji wa miaka minane labda ni utafiti mkubwa zaidi na wa kina zaidi wa mtu binafsi ulimwenguni.”

Cai ameongeza kuwa, “kulikuwa na tafiti nyingi hapo awali ambazo zilitoa uhusiano kwa muhtasari kati ya kelele za msongamano wa magari karibu na nyumba na hali ya shinikizo la damu kwa watu na hata hivyo, hakuna utafiti uliokuwa na ubora wa kutosha kusogeza mbele ajenda ya sera.”

Aidha, ameongeza kuwa, ushahidi unaonyesha upo uwezekano wa uhusiano kati ya kelele za msongamano barabarani na shinikizo la damu, uchafuzi wa hewa na sababu zingine za hatari na kwamba jambo hilo linakwenda kubadilisha hali linapokuja suala la kuzuia shinikizo la damu kwa mtu binafsi na kwa jamii.

“Ingawa ushahidi zaidi unahitajika, hii haipaswi kuchelewesha hatua ili kutambua kwamba kelele za magari ni sababu ya hatari ya shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo na kwa ujumla katika maendeleo ya mwongozo wa afya na sera za mazingira,” amebainisha Cai.


Maafisa watakao husika na ufisadi kufungwa jela

Hata hivyo, Mwandishi Mkuu wa utafiti huo Jing Huang, Profesa Msaidizi katika Idara ya Sayansi ya Afya Kazini na Mazingira katika Shule ya Afya ya Umma katika Chuo Kikuu cha Peking huko Beijing, China amesema “tulishangaa kidogo kwamba uhusiano kati ya kelele za barabarani na shinikizo la damu ulikuwa madhubuti na thabiti hata baada ya uchafuzi wa hewa kurekebishwa.”

Aidha, Watafiti hao walichambua data kutoka kwa zaidi ya watu 240,000, wenye umri wa kati ya miaka 40 hadi 69 ambao walianza kufuatiliwa wakiwa hawana shinikizo la damu au presha na kwa kutumia takwimu na data waliwafuatilia kwa wastani wa miaka 8 na mwezi mmoja, waliangalia ni watu wangapi walipata shinikizo la damu.

Aidha, waligundua pia watu wanaoishi karibu na kelele za barabarani walikuwa na kwenye hatari kubwa ya kupata shinikizo la damu, lakini pia hatari hiyo iliongezeka kila “makekele yalipozidi na kuwa mengi.

Maafisa watakao husika na ufisadi kufungwa jela

Hata hivyo, watu ambao walikuwa karibu zaidi na kelele za barabarani na kwenye uchafuzi wa hewa walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kupata shinikizo la damu, hii ni kuonyesha kuwa uchafuzi wa hewa una jukumu pia.

Watafiti walisema matokeo hayo yanaweza kusaidia hatua za afya ya umma kama vile kuweka miongozo mikali dhidi ya kelele za barabarani na kuboresha teknolojia kwenye magari ili yasipige kelele na kuimarisha muundo ya maeneo ya mijini.

Chanzo BBC Swahili.

GGML yaibuka kampuni kinara inayozingatia malengo ya SDGs
Kocha Geita Gold atangaza hatari Ligi Kuu