Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitaka Jumuiya ya kimataifa kulaani vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na serikali ya Rwanda dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali hiyo.

Aidha, katika Taarifa iliyotolewa na shirika hilo la haki za binaadamu na kusambazwa kwa vyombo vya habari imesema kuwa ukandamizaji huo unaofanywa na serikali ya Rwanda unamaanisha kuwa utawala huo hauko tayari kuwavumilia wakosoaji wake au kukubali dhima ya vyama vya upinzani.

Mkurugenzi wa shirika hilo ukanda wa Afrika ya Kati, Ida Sawyer, amesema kuwa hatua hizo za serikali ya Rais Kagame zinakusudiwa kutuma ujumbe wa vitisho kwa wale wanaojaribu kuukosoa utawala

“Katika kila mtu mmoja anayekamatwa nchini Rwanda, ni watu wachache sana wanaothubutu kuzungumzia dhidi ya sera ya dola au mateso wanayoyapata hivyo wanazidi kupungua,” amesema mkurugenzi huyo.

Hata hivyo, miongoni mwa watu waliokamatwa  hivi karibuni na Serikali ya Rwanda, kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo imemtaja aliyekuwa mgombea urais kwenye uchaguzi uliopita Bi Diane Rwigara, pamoja na familia yake na wafuasi wao, sambamba na viongozi kadhaa wa chama cha upinzani cha FDU-Ikingi.

Video: Mjadala wa maudhui ya kanuni za mitandao na utangazaji waanza
Mwanafunzi wa darasa la tatu apewa ujauzito, Kilombero