Kama ulikuwa mtazamaji mzuri wa kipindic ha ‘Vitimbi Show’ cha Mzee Ojwang wa Kenya, unaweze kupikicha macho yako mara 3000 ukiisoma post ya Huddah Monroe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kujaribu kumkumbuka kama ulimuona ‘Kayai’.

Kwa sababau eti Huddah aliwahi kuigiza kama mtoto wa marehemu Mzee Ojwang, ‘Kayai’ alipokuwa na umri wa mika 16!

Huddah ameweka ujumbe wake kwenye Instagram kutoa pole na kuonesha jinsi anavyomkumbuka Mzee Ojwang na kueleza kuwa aliwahi kuigiza kwenye ‘Vitimbi’ kama ‘Kayai’ ila wengi hawakujua.

“RIP Mzee Ojwang…… I remember days when I acted as Kayai on Vitimbi, stuff only a few people know. He was the funniest, humble guy I’ve ever met …….RIP legend, we will miss you. #16WasAGoodYear #TheHustleWasReal,” aliandika Huddah.

Hata hivyo, wapenzi wa show hiyo walionesha kumshangaa na kumtaka kuacha kutafuta stunt kwa marehemu.

“yaani she has to stunt even on RIP post.” Aliandika beausheilla.
“Just curious, which year was this, nilikua sijaanza kuangalia vitimbi ama??? I never saw kayai aki.” Aliandika naenci.

Man City Wamaliza Mzizi Wa Fitna, Wamsajili Rasmi Sterling
Mzee Yusuf Apanga Kuacha Muziki Ili Afanye Siasa