Milipuko chini ya Bahari ya Baltic, imepasua mabomba makubwa ya gesi asilia ya kutoka Urusi kwenda Ujerumani, ikidaiwa kusababishwa na shambulio la makusudi na kuzidisha kutokuwa na uhakika juu ya usalama wa nishati ya Ulaya huku bei ya hitaji hilo ikipanda na hofu ya kukosa mafuta wakati wa msimu wa baridi ikiongezeka.
Uvujaji wa gesi hiyo, uliotokea katika maeneo matatu tofauti umetokea kwenye mabomba ya Nord Stream 1 na 2, ambayo tayari yalikuwa yamenaswa katika mzozo wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, na kutuma vijito vinavyozunguka vya methane kwenye uso wa maji kutoka Denmark na Uswidi.
Viongozi wakuu wa Poland na Ukraine, waliilaumu Moscow, huku vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vikisema Marekani au Ukraine wanahusika katika sakata hilo, la mabomba hayo ambayo ni kitovu cha mzozo mkubwa kati ya Urusi na Ulaya.
Baada ya E.U. kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi, Moscow ilianza kuzuia gesi yake asilia, na kutishia usambazaji wa nishati ya bara hilo ambapo C.I.A. walitoa onyo lisilo wazi Juni, 2022 kwa mataifa kadhaa ya Ulaya, ikiwemo Ujerumani, kwamba mabomba mawili ya gesi ya Nord Stream ambayo hubeba gesi asilia kutoka Urusi yanaweza kushambuliwa.
Makubaliano yanayowezekana kati ya Israeli na Lebanon, ambayo kitaalam yamekuwa kwenye vita tangu 1948, yanaweza kuongeza uzalishaji wa gesi asilia, kusaidia Ulaya yenye uhaba wa nishati.