Baada ya siku 735 za mwenendo wa kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema, leo Machi 10, 2020 hukumu ilitarajiwa kutolewa asubuhi katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, lakini imepelekwa mbele hadi saa saba mchana huku Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akiandika ujumbe wa kuwaaga wananchi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hukumu hiyo inakuja baada ya February 24, 2020 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kutoa siku tano za kazi kwa Mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho kwenye shauri .

Jeshi lathibitisha Mangula kuwekewa Sumu, mhusika kusakwa

Mdee ameandika “Wakuu salaam!! Kesho Asubuhi ni siku ya HUKUMU ya Kesi ya VIONGOZI wa Chadema na MIMI nikiwa mmoja wapo.Chochote kinaweza kutokea !!Nimewiwa kutumia nafasi hii kuwaaga RASMI. Itoshe tu kusema, binafsi nimejiandaa kiroho SAFI KABISA KUKABILIANA na chochote kitakacho kuja”

Viongozi wanaokabiliwa na shauri hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, na Wabunge John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, John Heche, Peter Msigwa na pia aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema kabla ya kuhamia CCM, Vicent Mashinji.

Mgonjwa wa kwanza wa Corona afariki Afrika

Washtakiwa wote kwenye shauri hilo namba 112 la mwaka 2018 wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo kufanya kusanyiko na maandamano kinyume cha sheria na kutoa maneno ya uchochezi.

Mikutano ya SADC ana kwa ana yasitishwa
Jeshi lathibitisha Mangula kuwekewa Sumu, mhusika kusakwa