Kufuatia kesi iliyokuwa inawakabili wasanii wa muziki wa dansi nchini ambao walihukumiwa kifungo cha maisha jela, Papii Kocha na Nguza Viking, Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) kesho Machi 23, itawasomea hukumu ya kesi yao, kutokana na wawili hao kutofuata taratibu za kisheria mara baada ya kupata msamaha wa Rais, John Pombe Magufuli.

Mahakama hiyo imefanya maamuzi hayo mara baada ya wasanii kutoiandika barua ya kuarifu kuwa wamesitisha zoezi la dhamana waliyoiomba pindi wanapinga hukumu yao ya kifungo cha maisha jela  kufuatia kesi iliyokuwa inawakabili ya kunajisi na kulawiti watoto.

Hivyo mahakama imesema itaendelea na kazi yake kama kawaida na ikiwa watakutwa na hatia au laa kwamba jambo lao limeshapata msamaha na msamaha wa rais huwezi k uhojiwa popote.

”Hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji kwa sababu kile kifungo kimeshabatilishwa tayari”

Hayo yamesemwa na Jaji Sylvaine Ore ambaye ni rais wa AFCHPR, kutoka nchi ya Ivory Cost, ambaye ameahirisha kusoma hukumu hiyo leo, kutokana  na wawili hao kutoonekana mahakamani.

Hata hivyo, mwanasheria Daniel Kalasha ametoa maoni yake kuhusiana na hukumu hiyo amesema vyovyote itakavyokuwa hukumu hiyo haiwezi kuathiri msamaha wa rais waliopata, lakini walipaswa kuitaarifu mahakama kuachana na kesi hiyo kutokana na sababu hizo.

 

TANESCO yakanusha taarifa iliyozagaa mitandaoni
TFF yaanza Mchakato wa kumpata Kocha mpya Taifa Stars.