Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepokea taarifa ya Kamati ya Maadili ya Bunge ambayo iliketi kwa ajili ya kumhoji Mbunge wa Shinyanga Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika PAP.

Taarifa ya hukumu hiyo imewasilishwa bungeni jijini Dodoma hii leo na Mbunge Almas Maige ambaye amewasilisha ripoti hiyo wakati wa kikao cha Bunge.

“Kwa niaba ya Mwenyekiti Kamati ya Maadili ya Bunge, naomba kuwasilisha mezani taarifa kuhusu Mbunge wa Shinyanga Mjini, Julius Masele ya kulidharau Bunge, Mamlaka ya Spika, kulifedhesha Bunge na kuchonganisha mihimili ya dola,” amesema Maige.

Aidha, Mei 16, 2019, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliibua madai kuhusiana na Mbunge huyo kwa kile alichokidai kuwa amekuwa na utovu wa nidhamu.

“Nimemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wake, hadi Kamati ya Maadili itakapo kamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, na hapa kuna kamati mbili zinamsubiri ikiwemo Kamati ya Maadili ya Bunge na Kamati ya Maadili ya chama chake,” amesema Ndugai.

Spika Ndugai alisema kuwa, Stephen Masele ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyo hovyo, ndiyo maana wameamua kumuita ili aweze kufafanua huenda yuko sahihi, lakini anafanya mambo ambayo ni hatari kubwa, amekuwa akichonganisha mihimili miwili, na amejisahau sana.

Mbunge huyo Masele amehukumiwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kufuatia kosa lake hilo alilofanya.

 

Trump, Spika watofautiana, asusia kikao
Kundi la IS latua DR Congo, ukanda wa maziwa makuu waitisha kikao cha dharula

Comments

comments