Mtuhumiwa wa mauaji ya mwanamziki Moses Seskibogo (Mowzey Radio), Godfrey Wamala (Troy), amekutwa na hatia ya kumuua mwanamzki huyo bila kukusudia.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama kuu ya Entebee, Jane Abodo leo alhamis Octoba 31, na kusema kuwa mtuhumiwa huyo amekutwa na hatia ya mauaji ya bila kukusudia.

Jaji Abodo amesema Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 14 jela Wamala lakini atatumikia kifungo cha miaka 13, miezi 3 na siku 4 baada ya kukaa mahabusu kwa mwaka1.

Aidha amesema kuwa rufaa juu ya hukumu hiyo iko wazi kama Wamala atakuwa hajaridhika na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo.

Ikumbukwe kuwa Mwanamziki Radio alifariki katika hospitali ya Case Jijini Kampala, Tarehe 1 mwezi wa pili 2018, ambako alikuwa amelazwa baada ya kupigwa na Godfrey Wamala hadi kupoteza fahamu akiwa kwenye klabu ya starehe ya De Bar, iliyopo Entebbe.

Mambo 9 watu wenye akili hufanya zaidi
Jurgen Klopp: Sitapeleka timu uwanjani