Ni kweli kwamba kila mtu katika maisha hufanikiwa kwa namna yake, usitegemee jinsi alivyofanikiwa juma vivyo hivyo nawe utafanikiwa la-hasha.
Kwa tafsiri hiyo haina maana kuwa hatupaswi kuiga, kuangalia au kusikiliza waliofanikiwa walifanya vitu gani kuyafikia mafanikio hayo kwa imani kuwa kila mtu ana njia zake kuyafikia mafanikio, ijapokuwa kwa mtazamo wa msanii wa muziki ambaye ni msomi hapa nchini mwenye uwezo mkubwa kifikra na kujenga hoja amewahi kusema haamini katika kusoma vitabu wala kusikiliza wahamasishaji akiamini kuwa kwa kufanya hivyo unaweza kujikuta unapata mambo mengi kwa wakati mmoja na kuacha jambo la msingi.
Kwa mtazamo chanya kuna nguvu kubwa ya neno la uhamasishwaji, kuna nguvu kubwa katika kuona, kujifunza na kusikiliza ya wale waliotangulia katika safari ya mafanikio ili hali kuwa na wewe una safari yako.
Wengi hupenda kujifunza kwa kusoma vitabu mbalimbali vinavyohamsisha juu ya mafanikio na kuambulia chochote kitu katika kuisongesha safari hiyo.
-
Makala: Jitambue, tambulika, fahamu undani wa ubunifu wa mavazi
-
Wanasaikolojia wabaini hili katika mahusiano na uchepukaji njia kuu
Hivyo basi, jambo kubwa na la msingi kuliko yote katika safari ya mafanikio ni kuwa na nguvu za kusonga mbele, jitihada katika lile unaloliamini, kutokata tamaa haijalishi ni mara ngapi umeshindwa, uthubutu wa kufanya kitu bila kuogopa kushindwa.
Wengi wetu safari zetu huishia kati kwa kuogopa kuchekwa na kunyooshewa vidole, amini kila jambo na wakati wake, wakati mgumu ndio ukingo wa mafanikio.
Usithubutu kujilinganisha na mtu yeyote, wala kulinganisha mafanikio yako na mafanikio ya mtu mwingine, amini kile unachokifanya ni sahihi na kifanye kwa moyo na juhudi, wazungu wanasema ”time dont lie, it will tell” yaani muda hauongei unasema wakati ukifika.