Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesharuhusu usafirishaji wa makinikia baada ya kuweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji mapato amesema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo Bungeni leo, Waziri Mkuu amesema sheria imewekwa vizuri na kumekuwa na udhibiti wa kutosha ili kutokupoteza mapato.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Idd Kassim, mbunge wa Msalala (CCM) ambaye ametaka kujua Serikali ilizuia usafirishaji wa makinikia na nini kimesababisha kuanza tena kuyasafirisha kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu amesema Serikali ilisitisha usafirishaji wa makinikia tangu 2017/18 kutokana na kubaini kulikuwa na wizi na udanganyifu.

Amesema zuio hilo lililenga kufanya uchunguzi wa kujiridhisha na kutaka ianzishwe kampuni ya wazawa ambapo ilianzisha Kampuni ya Twiga ambayo Serikali ina ubia.

Waitara awasimamisha kazi vigogo wawili TPA
Aliyemshtaki Mungu Mahakamani bado anaishi