Essam El Hadary ni miongoni mwa magolikipa bora wa Afrika na natarajia kushiriki michuano ya kombe la dunia 2018 baada ya kuiongoza Misri kufuzu kufuatia ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mlinda mlango huyo anatarajiwa kuwa mchezaji mwenye umri kubwa zaidi katika fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Russia, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na raia wa Columbia Faryd Mondragon ambaye alikuwa na miaka 43 alipocheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil.

Essam El Hadary ataivunja rekodi hiyo na kuweka rekodi yake ambapo atakuwa na miaka 45 wakati wa fainali zijazo za kombe la dunia 2018 lakini hiyo itakuwa endapo atafanikiwa kucheza katika fainali zijazo za kombe la dunia.

Msindi huyo wa mataji manne ya Afrika aliyoshinda mwaka 1998, 2006, 2007 na 2010 amesema atapambana kuhakikisha anacheza fainali za kombe la dunia.

Essam alikuwepo kwenye kikosi kilichoshiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu akiwa ni mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi.

Wanaowania tuzo ya Ballon d'Or waanza kutajwa
Salah aibuka shujaa Misri, Didier Drogba amtumia ujumbe mzito