Kadri siku zinavyozidi kusogea, mtandao wa kijamii wa picha wa Instagram unazidi kupata umaarufu mkubwa huku watu maarufu wakishindana kuvuta idadi ya wafuasi, mwimbaji wa kike wa pop, Tailor Swift amefunika zaidi.

Jana, Tailor Swift alivunja rekodi na kuwa mtu maarufu zaidi duniani kwenye Instagram baada ya kufikisha ‘followers’ milioni 50.

Tailor SWIFT t

Washindani wa Tailor Swift ni warembo wenye umaarufu mkubwa, Kim Kardashian ambaye anajiita ‘Malkia wa Selfie’ ila sasa sio malkia wa Instagram kwa kuwa anashika nafasi ya pili akiwa na followers milioni 48.4.

Beyonce anashika nafasi ya tatu akiwa na followers milioni 47.5 huku nafasi ya nne na tano zinashikwa na warembo Selena Gomez akiwa na followers milioni 46.2 na Ariana Grande mwenye followers milioni 44.9.

Katika kusherehekea ushindi huo, Tailor Swift anayewafuata watu 78 tu, amepost kwenye Instagram ujumbe kuwashukuru mashabiki wake.

50 million followers!! Thanks so much guys. I’m pretty sure this is just because I have cute cats though. ?

A photo posted by Taylor Swift (@taylorswift) on

Mama Kim K Asimulia Alivyofanya Mapenzi Kwenye Ndege Halafu Mhudumu Akatangaza
Esther Bulaya Ashtakiwa Kwa Jaribio La Kuvamia Kituo Cha Polisi, Alazwa Selo