Meneja wa klabu ya Queens Park Rangers Ian Holloway, amemshukia mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na kumuita mbinafsi asievumilika.
Holloway ameibuka na kumshukia mshambuliaji huyo, baada ya kufuatilia kwa kina taarifa zake, kuhusu ugomvi aliouzua mazoezini dhidi ya wachezaji wenzake sambamba na kubwatukiana na meneja wake Arsene Wenger juma lililopita.
Alexis pia alionyesha kupokea tofauti maamuzi ya meneja wake baada ya kutolewa nje wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Swansea City, huku akionyesha kihoja kingine cha kucheka hadharani wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Bayern Munich uliomalizika kwa Arsenal kukubali kichapo cha mabao matano kwa moja.
Holloway alihojiwa na tovuti ya talkSPORT na kusema: “Imekua ni kawaida kwa mchezaji huyu kuonyesha vihoja dhidi ya wengine, na wakati mwingine anafika mbali kwa kuhisi ni mbora kushinda mtu yoyote, yeye ni nani hadi afikie hatua hii? Kwangu mimi ninamuita mbinafsi,”
“Amekua anaweka watu katika hali ya kufikiria kila kukicha kwa kuzua majanga ambayo hayavumiliki, kuna mengine anayafanya bila jamii kuyaona, lakini kwa haya ambayo tumeyaona hadharani tunapaswa kuyasemea ili ajirekebishe.
“Haiwezekani unafika katika hatua ya kuhisi wachezaji wenzako sio lolote si Chochote na kugombana nao, haitoshi unamvunjia heshima meneja wako, jambo hilo ningelikua mimi nisingelivumia hata kidogo!