Gwiji wa soka wa klabu ya Arsenal, Ian Wright ameshangazwa na mamauzi ya meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger, ya kumchezesha mlinda mlango kutoka nchini Colombia David Ospina katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambapo The Gunners walikubali kibano cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa mabingwa wa soka nchini Ugiriki Olympiacos.

Wright alizungumza kushangazwa kwake bila uwoga alipokua akichambua mchezo huo kupitia kituo cha televisheni cha BT Sports, na alisisitiza kutoamini maamuzi ya Wenger ambayo yameigharimu timu ya Arsenal.

Amesema mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, hakupaswa kumtumia mlinda mlango huyo, kutokana na kutoonyesha utayari wa kupambana katika michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hasa baada ya kucheza chini ya kiwango katika mpambano wa mzunguuko wa kwanza wa hatua ya makundi ambapo Arsenal walikubali kupoteza mbele ya Dynamo Zagreb.

Amesema David Ospina bado ni kipa mwenye vigezo vya kuitumikia Arsenal, lakini tangu aliporejea kutoka nchini Colombia baada ya michuano ya Copa America amekua na hali ya kutokujiamini kama ilivyokua msimu uliopita, hali ambayo kwake amesisitiza kuwa chanzo cha kushindwa kufanya vyema.

Katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, Ospina alionyesha udhaifu mkubwa kwa kuutumbukiza langoni mpira aliokua ameshaudaka, na matokeo yake aliwazawadia wageni bao la pili miongoni mwa mabao yao matatu yaliyowapa ushindi kwenye uwanja wa Emirates.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Champions League – Group E

BATE Borisov 3 – 2 Roma

Barcelona 2 – 1 Bayer Leverkusen

 

Champions League – Group F

Arsenal 2 – 3 Olympiakos

Bayern Munich 5 – 0 Dinamo Zagreb

 

Champions League – Group G

FC Porto 2 – 1 Chelsea

Maccabi Tel Aviv 0 – 2 Dynamo Kyiv

 

Champions League – Group H

Lyon 0 – 1 Valencia

Zenit St. Petersburg 2 – 1 Gent

 

Michuano hiyo inaendelea tena hii leo.

Champions League – Group A

Malmoe FF VS Real Madrid

Shakhtar Donetsk Vs Paris Saint Germain

Champions League – Group B

CSKA Moscow VS PSV Eindhoven

Manchester United Vs Wolfsburg

 

Champions League – Group C

FC Astana Vs Galatasaray

Atletico Madrid Vs Benfica

 

Champions League – Group D

Borussia Moenchengladbach Vs Manchester City

Juventus Vs Sevilla

 

 

Jaji Lubuva Aziba Mwanya Mwingine Wa Wizi Wa Kura
Nyosso Atupwa Jela Miaka Miwili