Mshambulizi wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG), Zlatan Ibrahimovic ametanabaisha kuwa siku moja angependa kuchezea klabu ya Bayern Munich kabla ya kustaafu soka.

Msweden huyo ambaye ni muongeaji mzuri, mara kadhaa amedaiwa kutaka kurudi AC Milan katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto, huku rais wa Milan Silvio Berlusconi akikiri kuwa bado wana uhitaji mkubwa wa kumnasa mshambulizi huyo licha ya ujio wa Mbrazil Luiz Adriano na Carlos Bacca.

Hata hivyo, Ibrahimovic amebainisha kwamba angependa kujaribu kucheza ligi nyingine kabla ya kustaafu, huku akikiri Bayern Munich ndio timu pekee kwa sasa ambayo angependa kuchezea.

“Kiukweli kwa kiasi fulani ndio ligi inayonivutia kwa sasa, “aliiambia 11Freunde. “Pengine siku moja naweza kucheza pale, Bado muda upo.”

“Kama nikienda Ujerumani, ningependa kukipiga Bayern, ni miongoni mwa timu tano bora duniani,” anakaririwa.

Kwa upande mwingine, uwezekano wa Zlatan kwenda Bayern unaweza kuwa mgumu kutokana na uwepo kwa Pep Guardiola, ambapo

wote hawana maelewano mazuri.

Rais Kikwete Aumizwa na Vichapo Vya Taifa Stars
Ndugu wa Kim Kardashian apozi mtupu kuuza bidhaa za ‘Calvin Klein’