Uongozi wa Klabu ya Coastal Union umeweka imani yao kwa kiungo Ibrahim Ajibu waliyemsajili kwa mkopo akitokea klabu ya Singida Fountain Gate.

Afisa Habari wa Coastal Union, Jonathan Tito amesema Ajibu ni mchezaji mzuri na uzoefu wake utaisaidia timu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara ambao wameweka malengo ya kufanya vizuri.

“Sio mchezaji mbaya sote tumemshuhudia huko alikotoka. Tunaamini ataongeza nguvu na kuisaidia timu,” amesema Tito.

Tito amesema wanaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa ligi chini ya kocha wao mpya Mwinyi Zahera aliyechukua nafasi ya Fikirini Elias.

Mbali na Ajibu, wengine waliosajiwa na timu hiyo mpaka sasa ni beki Abdallah Denis kutoka Malindi ya Zanzibar, Lucas Kikoti kutoka Namungo FC na Ally Kombo kutoka Ruvu Shooting.

Jeshi lapanga mkakati kuingilia kati Sakata la Niger
Upatikaji wa Dola: Serikali iongeze jitihada - TAOMAC