Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Ibrahim Class ameingia kambini kujiandaa na pambano dhidi ya Xion Tau Su kutoka China.
Pambano hilo lisilo la ubingwa litafanyika Oktoba 28, mwaka huu katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.
Akizungumza Dar es salaanm, Ibrahim Class amesema pambano hilo litakuwa gumu kwake kwani mabondia wengi kutoka China wamekuwa na uwezo mkubwa.
“Nimeingia kambini kujinoa chini ya kocha wangu Habibu Kinyogoli, mashabiki na watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwangu,” amesema.
Class amesema atajituma vyema mazoezini kuhakikisha anakuwa fiti kumchakaza mpinzani wake.
Mbali na pambano la lbrahim Class, mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni Mtazania Fadhili Majiha dhidi ya Bongani Mahlangu kutoka Afrika Kusini.
Nassib Ramadhani atazichapa na Zolisa Batyi (Afrika Kusini), huku Stumani Muki akivaana na Loveleen Thaakur kutoka India.