Kiungo wa klabu ya Slavia Prague Ibrahim Traore ametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast, ambacho kitaanza kampeni ya kuwania kufuzu fainali za Afrika 2021 (AFCON 2021) mwezi huu.
Traore ametajwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha taifa hilo akiwa na umri wa miaka 31, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa ambao umemvutia kocha mkuu Ibrahim Kamara.
Ivory Coast itaanza kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika 2021, kwa kupambana na Nigeria Novemba 16, na siku tatu baadae itakutana uso kwa macho na Ethiopia.
Traore, ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Slavia Prague kilichotwaa ubingwa wa ligi ya Jamuhuri ya Czech msimu uliopita, jana jumanne alicheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona, ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Msimu huu wa 2019/20, kiungo huyo ameshaitumikia klabu yake katika michezo tisa, na kufunga bao moja.
Neya mshambuliaji wa Olympic Lyon ya Ufaransa Maxwel Cornet na kiungo Christian Kouame anayeitumikia klabu ya TP Mazembe, wote kwa pamoja wametajwa kwenye kikosi cha Ivory Coast.
Gervinho ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Parma ya Italia bado anaendelea kufuatiliwa kwa ukaribu na kocha Kamara, kama ilivyo kwa Jonathan Kodjia wa Aston Villa na Jean Michael Seri wa Galatasaray.
Kikosi cha wachezaji 24 kilichotajwa na kocha Ibrahim Kamara.
Makipa: Gbohouo Sylvain (TP Mazembe, DR Congo), Badra Ali Sangare (Uthongathi FC, South Africa) na Sayouba Mande (Odense BK, Denmark).
Mabeki: Serge Aurier (Tottenham Hotspur, England), Britton Willie (FC Zurich, Switzerland), Ghislain Konan (Reims, France), Wonlo Coulibaly (TP Mazembe, DR Congo), Ismael Traore (Angers, France), Wilfried Kanon (Pyramids FC, Egypt), Cheick Comara (Wydad Casablanca, Morocco) na Simon Deli (Club Brugge, Belgium).
Viungo: Franck Kessie (AC Milan, Italy), Seko Fofana (Udinese, Italy), Habib Maiga (Metz, France), Christian Kouame Koffi (TP Mazembe, DR Congo), Ibrahim Traore (Slavia Prague, Czech Republic) na Victorian Angban (Metz, France).
Washambuliaji: Wilfried Zaha (Crystal Palace, England), Nicolas Pepe (Arsenal, England), Max Gradel (Toulouse, France), Roger Assale (Young Boys, Switzerland), Yohan Boli (Saint Truidense, Belgium), Maxwel Cornet (Lyon, France) na Yakou Meiti (Reading, England).