Beki wa kati wa Liverpool, Ibrahima Konate amekiri anahitaji kuongeza kiwango zaidi anapojiandaa kuanza msimu wake wa tatu na klabu hiyo.

Konate aliwasili hapo Liverpool kwa Pauni Milioni 36 msimu wa majira ya joto wa 2021 kutoka RB Leipzig.

Lakini mambo kwa Mfaransa huyo yamechukua muda alitumia muda mwingi wa kampeni yake ya kwanza kwenye benchi, wakati majeraha msimu uliopita yalimfanya asicheze mara kwa mara.

Lakini akiwa na umri wa miaka 24, amebakiwa na miaka mitatu kwenye mkataba wake, bado kuna uwezekano mkubwa kwa Konate kuendeleza kama inavyotarajiwa.

“Nina furaha sana kuwa hapa na ninataka kushinda mataji mengi na klabu hii kwa sababu ni klabu ya ajabu yenye historia kubwa,” aliiambia LiverpoolFC.com.

“Nataka kuwa sehemu kubwa ya klabu hii na kushinda mataji mengi nikiwa na klabu hii. Nadhani msimu huu, msimu wa tatu, lazima nijipange na kuonyesha haiba yangu nyingine uwanjani na maishani pia. Nina ma- lengo mengi.”

Aliyeitwa na Rais mara tatu bila kuitika apewa ukamanda
Maafande wampa kiburi Minziro, achimba mkwara