Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amejumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kitakacho shiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya katika ngazi ya makundi.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 aliachwa na Man United baada ya kupata maumivu ya goti mwezi Aprili lakini amejiunga tena na klabu hiyo na atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaounda kikosi kitakacho shiriki katika michuano ya UEFA.

Awali kocha wa Manchester United Jose Mourinho alionyesha kuwa Zlatan asingeweza kuwa katika kikosi chake kitakachoshiriki katika Michuano ya klabu bingwa ngazi ya makundi lakini Zlatan amepona mapema na ataungana na kikosi cha Man Utd.

”Sidhani kama tutakuwa naye katika ngazi ya makundi nafikiri anaweza kujiunga na timu katika ngazi ya mtoano akiwa amepona” alisema Jose Mourinho.

Msimu uliopita Ibrahimovic alifanikiwa kuifungia Man United jumla ya mabao 28 na kuiwezesha timu hiyo kushinda kombe la Europa league pamoja na kombe la EFL.

Man United wataanza michuano ya klabu bigwa kwa kuwavaa FC Basel tarehe 12 mwezi Septemba kabla ya kucheza na CSKA Moscow tarehe 27 mwezi Septemba na Benfica tarehe 18 mwezi Octoba.

 

Marekani yaishangaa Korea Kaskazini kutaka vita
Wachezaji Arsenal wamkera Petit