Mwendesha mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Karim Khan ameushutumu Umoja wa Ulaya kutoa pendekezo la kuunda Mahakama maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kushtaki uhalifu unafofanyika nchini Ukraine.
Khan anasema, Mahakama yake ina uwezo wa ufanisi kushughulikia uhalifu wa kivita unaofanywa huko na kwamba kufungua korti nyingine ni matumizi mabaya ya pesa na rasilimali watu hivyo badala ya kufanya hivyo ni vyema wakaelekeza nguvu hizo kwenye mambo mengine.
Haya hivyo, inadaiwa kuwa Umoja wa Ulaya umeteleza kisheria katika maamuzi hayo na kwamba taasisi yake inawezo ya kuwashtaki hata maafisa wa ngazi ya juu watakaotuhumiwa na huku hatua hiyo ikimuonesha Khan kama anapingana na mpango wa Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.
Ursula von der Leyen, ajuma lililopita alisema kuundwe Mahakama maalumu itakayohusika na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kuelekeza Mahakama ya ICC yenye makao yake mjini The Hague ianzisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Ukraine lakini haiwezi kushtaki uhalifu wa kuvamia nchi nyingine kwa taifa kama Urusi kwa kuwa taifa hilo sio sehemu ya mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo.