Sare ya bila kufungana iliyopatikana kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya kati ya Iceland dhidi ya Kazakhstan imetoa mtazamo chanya katika msimamo wa kundi la kwanza.

Matokeo hayo yameiwezesha timu ya taifa ya Iceland kufuzu kucheza fainali hizo za mwaka 2016 ambazo zitaunguruma nchini Ufaransa, baada ya kufikisha point 19 sawa na Jamuhuri ya Czech.

Iceland walifanikisha matokeo hayo ya sare wakiwa nyumbani na sasa watacheza michezo miwili iliyosalia kwenye kundi hilo bila ya kuwa na mshawasha wa kupoteza ama kutoka sare kutokana na lengo lao kutimia.

Hata hivyo kwa sasa Iceland wapo kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa na endapo watahitaji kujiimarisha kwenye nafasi hiyo itawalazimu kusaka ushindi katika michezo yao iliyosalia ambapo watapambana na Latvia Oktoba 10 na kisha watamalizia kampeni ya kuelekea nchini Ufaransa kwa kupambana na Uturuki Oktoba 13.

Jamuhuri ya Czech nao wamefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali za mwaka 2016, na itawalazimimu kusaka nafasi ya kwanza ama ya pili katika kundi hilo kufuatia uwiyano sawa wa point uliopo hivi sasa dhidi ya Iceland.

Katika kundi hilo la kwanza zipo timu za taifa za Uholanzi pamoja na Uturuki ambazo zilikua zikipigia chapuo la kufuzu wakati kampeni hizo zilipoanza mwaka 2014, lakini zimeonyesha kushindwa na kwa sasa zinasubiri kudra za kucheza michezo ya hatua ya mtoano.

Timu nyingine zilizopo kwenye kundi hilo ni Latvia pamoja na Kazakhstan.

Timu nyingine iliyofanikiwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya mpaka sasa ni England iliyofikisha point 21 katika msimamo wa kundi la tano ikiziacha timu za Uswiz, Estonia, Slovenia, Lithuania pamoja na Sana Marino.

Katika kundi hilo Uswiz wanaonyesha dhamira ya kuwafuata England kwa kufikisha point 15 huku Estonia wakiwa kwenye nafasi ya tatu kwa kumiliki point 10.

England walijipatia tiketi ya kuelekea nchini Ufaransa wakiwa wamesaliwa na michezo miwili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri dhidi ya San Marino mwishoni mwa juma lililopita.

Michezo miwili ya kuhitimisha kwa England katika kundi la tano itakua dhidi ya Estonia kisha Lithuania itakayochezwa mwezi ujao.

Matokeo ya michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 iliyochezwa jana.

Latvia 1-2 Czech Republic

Turkey 3-0 Netherlands

Wales 0-0 Israel

Bosnia-Herzegovina 3-0 Andorra

Cyprus 0-1 Belgium

Malta 2-2 Azerbaijan

Norway 2-0 Croatia

Italy 1-0 Bulgaria

Lowassa Aiwekea CCM Mzani Kwa Wananchi
Klopp Avishukia Vyombo Vya Habari