Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya basi ya New Force iliyotokea katika Kijiji cha Igando kilichopo Kata ya Luduga Wilayani Wanging’ombe Mkoani wa Njombe imefikia saba na majeruhi 48.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, John Imori amesema waliofariki ni wanaume watano akiwemo dereva wa basi na mtoto na wanawake wawili.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni dereva basi hilo lenye namba za usajili T 173 DZU kujaribu kulipita lori bila ya kuchukua tahadhari.

Basi hilo la New Force lilikuwa likitoka Mkoani Dar es salaam kuelekea Rukwa, na lilipofika eneo la Igando sehemu yenye daraja dereva alitaka ‘kuovartake’ ndipo likapoteza uelekeo na kugonga daraja kisha kuangukia mtaroni.

Asimulia mwanaye alivyosajiliwa kumuabudu shetani
Maofisa wa Serikali kizimbani kwa kusema uongo