Zaidi ya watu 600 wamekufa katika mfululizo wa matukio ya mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika muongo mmoja nchini nchini Nigeria, ambayo yamewalazimu zaidi ya watu milioni 1.3 kuyahama makazi yao.
Waziri wa Masuala ya Kibinadamu wa Nigeria, Sadiya Umar Farouq amesema mafuriko hayo yameharibu pia zaidi ya nyumba 82,000 na karibu ekari 272,000 za mashamba kitu ambacho kinatoa ishara ya baa la njaa.
Eneo hilo, la Kusini mwa Jangwa la Sahara limeathirika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha mvua nyingi ambazo zimeleta maafa na bado zinaendelea kunyesha
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), kwa pamoja wamesema Nigeria ni miongoni mwa nchi sita zinazokabiliwa na hatari kubwa ya kukabiliwa na janga la njaa Duniani.