Idadi ya Wahamiaji wanaoelekea Ulaya, waliofariki au kupotea katika Bahari ya Mediterania msimu huu wa joto, imeongezeka mara tatu tangu mwaka jana 2022 na kwamba Bahari hiyo imegeuka kuwa “makaburi” ya watoto
Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, limesema kuanzia mwezi Juni hadi Agosti 2023, takriban watu 990 walikufa au kutoweka wakijaribu kuingia Ulaya kutoka kaskazini mwa Afrika, ikilinganishwa na vifo vya watu 334 katika kipindi hicho kwa mwaka 2022.
Mratibu wa UNICEF Nchini Italia, Nicola dell’Arciprete amesema mwaka 2023, takriban watoto 289 wamekufa kufikia sasa wakati wao na Wazazi wao walipokuwa wakijaribu safari hizo za hatari.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi – UNHCR, Wahamiaji wapatao 2,500 wamefariki au kutoweka katika Bahari ya Mediterania, katika kipindi cha Januari 1 hadi Septemba 24, 2023 ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganisha na mwaka 2023.