Idadi ya watu waliokufa, kutokana na mripuko uliotokea katika mgodi wa Makaa ya mawe Kaskazini mwa nchi ya Uturuki, imepanda na kufikia watu 40.

Shughuli za uokoaji, bado zinaendelea huku moto ukiwa bado unawaka katika mgodi huo ambapo takriban wafanyakazi 110 waliokuwa ndani ya mgodi huo wa TTK Amasra Muessese Mudurlugu unaomilikiwa na serikali, wakati mripuko ulipotokea.

Waziri wa nishati wa Uturuki, Fatih Durmaz amesema Juhudi zinaendelea za kuwafikia watu wengine 15 ambao wamekwama katika eneo linalowaka moto.

Amesema, “Moto sio mkubwa sana lakini ni lazima uzimwe pamoja na gesi ya Kaboni iliyo na sumu idhibitiwe kabla ya waokoaji kuendelea na operesheni yao,” huku Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan akitarajiwa kufika katika eneo la ajali hii leo Jumamosi Oktoba 15, 2022.

Wazee ni hazina MUNGU awabariki: Makamu Rais
Bilioni 2.2 wakabiliwa na uoni hafifu, upofu Duniani