Idadi ya wanafunzi waliopoteza maisha kwa mlipoko wa bomu mkoani Kagera imeongezeka mpaka kufikia wanafunzi tisa mpaka sasa.

Awali ililipotiwa kuwa idadi ya wanafunzi waliofariki kutokana na mlipuko huo ni wanafunzi sita huku majeruhi wengine wakiwa wamefikishwa katika Hospitali ya Rurenge kwa ajili ya matibabu wengi wa majeruhi wakiwa na hali mbaya.

Majeruhi waliofikishwa Hospitalini hapo wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha na wengine wameumia macho.

 

 

TFDA yazifutia usajili dawa zenye madhara kwa binadamu
Bomu laua wanafunzi sita Kagera