Scolastica Msewa, Mikumi – Morogoro.
Zaidi ya Watanzania 60,000 wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi katika kipindi cha Juni 2022 – June 2023 baada ya hamasa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya the Royar Tour, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka hadi Watanzania 100,000 kwa mwaka 2023/24.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati akiwapokea Wanachama 162 wa kikundi cha kufa na kuzikana cha Mlandizi family cha Kibaha Mkoani Pwani katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ignace Gara amesema awali Watalii walipungua kutokana na athari za Uviko-19.
Amesema, Watanzania kitendo cha Rais Samia kukuhamasisha utalii kwa njia ya Filamu kimesaidia ongezeko la Watalii wakiwemo wa ndani na kuwataka wanatakiwa wengine pia waige utamaduni huo ili kushuhudia vivutio vya kipekee nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Mlandizi Family, Eli Achahofu Paulo amesema kikundi chao kina wanachama kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani ambao husaidiana masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na misiba lakini awamu hii wameamua kufika mbugani hapo, ili kujionea kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt. Samia upande wa utalii.
Naye Msemaji wa kikundi cha Mlandizi family, Nyabhise Wandwi ameishauri serikali kuanzaisha utaratibu wa wanafunzi kuanzia shule za msingi za serikali kutembelea kwenye hifadhi za wanyama kujionea na kujifunza mengi kupitia utalii huo wa wanyama poli nchini.