Halmashauri ya jiji la Minneapolis katika jimbo la Minnesota nchini Marekani, imekubaliana kuivunja kabisa idara ya polisi na kuweka muundo mpya wa utendaji kazi wa polisi.
kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza la mji huo Lisa Bender, Idara ya polisi itafanyiwa mabadiliko makubwa kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd.
Floyd aliuawa mikononi mwa polisi wiki mbili zilizopita mjini humo tukio ambalo lilizusha maandamano ya kitaifa nchini Marekani na mengine mengi katika nchi mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa mwaka jana, afisa mmoja wa polisi wa zamani mjii Minneapolis alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na miezi sita jela kwa kumpiga risasi na kumuuwa mwanamke mweupe wa Australia ambaye hakuwa na silaha yoyote, wakati akitoa habari ya tukio la uhalifu.