Mshambuliaji wa Azam FC, Iddy Nado ameutazama msimu huu ulivyoanza na kusema umempa picha ya namna ambavyo anapaswa kujipanga kuhakikisha anakuwa na mchango kwa timu yake kumiliki mabao mengi.

Tayari amefunga bao moja katika Ligi Kuu Bara, timu yake ikiichapa Tanzania Prisons mabao 3-1 na Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF), kafunga moja, Azam ikitolewa kwa mikwaju ya Penati 3-4 dhidi Bahir Dar Kenema ya Ethiopia.

“Ni msimu mgumu unaohitaji kupambana, kwani mechi za mwanzo zimetoa taswira jinsi Ligi Kuu itakavyokuwa tafu, kama mchezaji najipanga ili niwe msaada kwa timu yangu,” amesema na kuongeza;

“Naona washambuliaji walivyoanza na kasi ya kucheka na nyavu, hilo linatoa chachu ya ushindani zaidi kwa kila mchezaji kuoyesha kiwango chake, ligi inavyokuwa nguvu ndivyo viwango vinavyozidi kupanda juu, kwani kila mmoja anakuwa anajituma kupambania timu yake.”

Amesema licha ya timu yao kutolewa hatua ya awali kwenye michuano ya CAF haiwafanyi walegeze kamba kwenye Ligi Kuu, badala yake wanapambania malengo makubwa waliyonayo.

“Tunajipanga na kikosi chetu kina ushindani kuanzia kwenye namba, hivyo itatusaidia kushindana hadi kwenye mechi.” amesema.

Rasmus Hojlund kuivaa Arsenal Jumapili
Cesc Fabregas azichambua Arsenal, Chelsea