Muigizaji, muongozaji na muandaaji wa filamu kutoka nchini Tanzania, Idris Sultan ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye matukio mbalimbali ya kimataifa, na weekend hii anatarajiwa kushiriki tukio lingine kubwa litakalomkutanisha na mastaa wengi maarufu duniani, akiwemo staa wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Nigeria pamoja na klabu ya Napoli ya nchini Italy, Victor Osimhen.

Mbali na Osimhen, tukio hilo linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Juni 15, 2024 katika uwanja wa Taifa wa Nigeria litashuhudia uwepo wa mastaa wengine wakubwa kama Cloud Makelele, Sol Campble, Khalilou Fadiga, Nwankwo Kanu, Louis Saha (mchezaji wa zamani wa Manchester United), na beki wa zamani wa Arsenal, Eboue.

Mbali na wanamichezo hao maarufu, watu wengine mashuhuri ambao watakua pamoja na Idris Sultan ni wachekeshaji wakubwa wakiongozwa na Ayodeji Makun maarufu kama ‘Aycomedian’, Funybone, pamoja na mchekeshaji Crazeclown Kutoka nchini Nigeria.

Idris Sultan anakua msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kupata mualiko huo mkubwa.

Wiki ya Utumishi: TASAF kuwajengea uelewa Wananchi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni 9, 2024