Msanii maarufu nchini Tanzania, Idriss Sultan ameamua kutii agizo la mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Maonda na sasa anashikiliwa na polisi jijini Dar es salaam baada ya kuvunja sheria za mtandaoni kwa kuweka picha yake katika mtandao wa kijamii huku picha hiyo ikiwa na sura ya rais Magufuli.
Idris Sultan alijisalimisha kituo kikuu cha polisi jijini Dar es salaam kisha kuhojiwa.
Kwa mujibu wa wakili wake Eliya Rioba, Idris amewajibishwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao kifungu cha 15 na 16 ambavyo vinaeleza kuhusu kutengeneza taswira ya kuigiza kwa kutumia kompyuta pamoja na kusambaza taarifa zenye uongo ndani yake.
Mchekeshaji huyo ambaye aliwahi kuwa mshindi wa kipindi cha televisheni cha uhalisia cha ‘Big Brother Africa’ Idris Sultan.
Picha hizo mbili zinaonyesha kichwa cha Magufuli katika kiwiliwili huku picha moja akiwa amevaa suti huku amekaa kwenye kiti cha rais na nyingine akiwa amesimama huku amevaa mtindo wa ‘suspender’.
Huku picha hizo zikiwa zinasindikizwa na ujumbe kuwa “Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani”.
Siku ya Jumanne, rais Magufuli alikuwa anasheherekea miaka 60 ya kuzaliwa, sherehe ambayo wananchi wa taifa hilo walitumia mitandao ya kijamii kwa wingi kutuma salamu zao kwa rais.
Aidha, viongozi na watu mbalimbali maarufu na mashuhuri akiwemo, Waziri Kigwangalla alijitokeza na kumkingia kifua Idriss Sultan na kudai kuwa alichokifanya ni katiak kuonyesha upendo siku ya Rais ya Kuazaiwa kama ambavyo watanzania wengine kwa namna tofauti walijaribu kufanya.
Havyo Kigwangalla alisema kuwa endapo Idriss atashikiliwa na polisi atajitolea mwanasheria wa kumsimamia katika shtaka hilo ambalo kwa upande wake hakuona kosa lolote alilotenda mchakeshaji huyo.
Hata hivyo kupitia mitandao ya kijamii wasanii mbalimbali akiwemo Billnas wameendelea kumtania Idriss kwa janga lililomkuta jambo ambalo ni kawaida kwani Billnas na Idriss ni watani wakubwa sana, ikumbukwe kuwe hata kipindi ambacho Billnas alipata mkasa mkubwa sana akiwa kwenye mahaba na Nandy Idriss alikuwa mtu wa kwanza kumtania.