Rapper wa kike kutoka Australia, Iggy Azalea amezitaka media kuacha kuchochea kuni na kumchonganisha na Britney Spears akisisitiza kuwa wawili hao bado ni marafiki.

Sintofahamu kati ya Iggy na Britney ilianza kuripotiwa na vyombo vya habari baada ya rapa huyo kueleza mtazamo wake kuwa anadhani wimbo wa Britney ‘Pretty Girls’ alioshirikishwa haukufanya vizuri kwenye charts kwa sababu ulikosa promo ya kutosha.

“Ni ngumu kuupeleka wimbo juu ya charts bila promo ya ziada na kucheza kwenye TV n.k, bahati mbaya mimi nimeshirikishwa tu,” inasomeka sehemu ya Tweet ya Iggy akijibu swali la shabiki, tweet iliyoibua zogo.

Iggy ambaye amerudi kutumia twitter hivi karibuni baada ya kuisusia kutokana na kushambuliwa na watu ametumia mtandao huo kueleza kwa kina jinsi alivyochukizwa na ripoti za media kuhusu suala hilo zikionesha kuwa wasanii hao hawaelewani tena.

“am honestly not surprised but still really saddened that the media is trying to create a “beef” between @britneyspears and myself.” Alitweet Iggy.

Katika tweet nyingine, Iggy amesema anadhani media inataka kuona wasanii wa kike wakigombana na kusisitiza kuwa hakuna mtu anaerusha madongo kwa mwenzake kati yake na Britney Spears na kwamba alichokisema awali kilikuwa mtazamo wake wenye lengo la kujenga na kwamba unaweza kutumika kwa wimbo wowote.

Wimbo wa Britney Spears ‘Pretty Girls’ aliomshirikisha Iggy Azalea umeshindwa kufanya vizuri kwenye charts kama wengi walivyotarajia na ilishika nafasi ya 29 katika Billboard Hot 100.

Vanessa Mdee Aeleza Jinsi Alivyosifiwa na ‘Jay Z’ Walipokutana
Picha: Chris Brown aonesha jumba jipya na tattoo mpya